Wavuvi watatu waokolewa Mombasa baada ya kukaa siku tatu baharini

MOMBASA

KENYA

18TH JANUARY 2023

 

Wavuvi watatu raia wa tanzania waliokolewa na meli ya mizigo baada ya kukwama baharini kwa siku tatu. Wavuvi hao walifika  salama katika bandari ya Mombasa Jumanne usiku. Polisi wanasema watatu hao wanatoka eneo la Tanagani Pemba na walikaa  bila chakula wala maji baada ya mtumbwi wao waliokuwa kwenye msafara wa uvuvi kupinduka kufuatia dhoruba kali. Watatu hao walikuwa wamefunga safari kuelekea bahari kuu mapema Jumamosi asubuhi mwendo wa saa nne asubuhi kwa mtumbwi usio na injini. Jumatatu jioni, nahodha wa meli kubwa aliona mtumbwi ukiwa na watu waliokuwa wamekwama ndani ya eneo la bahari la Kenya.

Nahodha huyo aliripoti kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari ya Kenya na akashauriwa kuwasaidia watatu hao na kuwafikisha Mombasa. Balozi wa Tanzania aliarifiwa mara moja na baada ya kuwahoji watatu hao, alibaini walikuwa raia wa Tanzania. mipango inaendelea kuhakikisha wanarejeshwa nyumbani.

Leave a Comment