
Mamia ya waandamanaji washika mabango barabarani, kupinga uwaniaji urais wa Seif Gaddafi na Halifa Haftar mjini Tripoli, Libya.
Tripoli, Libya
Mamia ya Walibya waliandamana jana Ijumaa mjini Tripoli kupinga kile walichokitaja kuwa wahalifu wa kivita kutaka kuwania urais nchini humo mwezi ujao.
Ni baada ya mbabe wa kivita anayeongoza vikosi vya mashariki ya nchi hiyo Khalifa Haftar pamoja na mwana wa rais wa zamani aliyeng’olewa mamlakani Muammar Gaddafi, Seif al-Islam kujitosa kwenye kinyanganyiro cha urais.
Waandamanaji waliobeba mabango ya Haftar na Seif Gaddafi walielezea ghadhabu zao kuhusu sheria tete ya uchaguzi ambayo inaepusha mchakato kamili na badala yake kumpendelea Haftar.
Mbunge mmoja nchini humo ametaka wale wote ambao wanahusishwa na uhalifu dhidi ya raia wa Libya wazuiwe kushiriki kwenye uchaguzi.
Libya, nchi ya upembe mwa Afrika imekuwa kwenye mzozo wa kisiasa tangu aondolewe madarakani Rais Muammar Gaddafi mwaka 2011.
Taarifa hii ni kwa hisani ya DW/20.11.2021