Picha/Umoja wa Mataifa

Kilifi, Kenya

Eneo bunge la Rabai na sehemu za Kilifi Kaskazini zinatajwa kupigwa hatua kubwa sana kutumia vyoo Kaunti ya Kilifi, Pwani ya Kenya.

Kulingana na sensa ya mwaka 2019, Kilifi iliorodheshwa miongoni mwa Kaunti 15 zenye changamoto kubwa ya kutumia vyoo nchini Kenya.

Mshirikishi wa afya ya umma Kaunti ya Kilifi Amos Ndenge ameambiwa idhaa ya Kiswahili ya SBS kwamba kufikia mwaka 2024, Kaunti ya Kilifi inatarajiwa kuwa na vyoo kwenye kila makaazi.

Wadi tano za Kilifi Kaskazini pia zinatajwa kuwa kwenye harakati za mwishomwomwisho kuwekwa kwenye orodha ya maeneo yanatumia vyoo kikamilifu.

Kwa sasa anasema ni eneo bunge la Rabai pekee ndilo linalotumia vyoo kikamilisha Kaunti ya Kilifi.

“Tunapambana sana kuhakikisha kila mtu hapa Kilifi anatumia choo, lakini pia serikali haitakuja kukuchimbia choo isipokuwa wewe mwenyewe uhakikishe unafanikisha hilo,” ameambia SBS Radio mapema leo Alhamisi.

Takwimu zinaonesha kuwa watu wapatao bilioni 4.5 kote Ulimwenguni hawana vyoo, na kiasi cha watoto 750 kote ulimwenguni hufariki dunia kila siku kutokana na maradhi ya kuharisha kwa kutumia maji chafu.

Maradhi haya wataalamu wanasema yanasabaishwa na kutotumia vyoo.

Ofisa Ndenge anasema serikali ya Kaunti inaendeleza hamasa kuhusu umuhimu wa kutumia vyoo kwa jamii.

Anawatolea wito wananchi kuhakikisha wanachimba vyoo na pia kuvitumia ili kujiepusha na magonjwa yanayosababishwa na uchafu.

Maeneo ya Ganze, Kaloleni na Magarini yanatajwa kuwa yangali na changamoto ya kutumia vyoo kutokana na Umaskini unayoyakumba.

Maadhimisho ya mwaka huu ya Siku ya vyoo Ulimwenguni itaadhimishwa katika shule ya msingi ya Majajani chini ya Kauli mbiu “Tunathamini vyoo.”

 

Mwandishi: David Charo Ngumbao,

Tarehe: 18.11.2021.

Saa: 18.11.2021

Mrejesho: Tutumie maoni yako

Leave a Comment