Kituo cha Mafuta. Picha/hisani

Nairobi, Kenya

Bei za mafuta ya Petroli, Diseli na ya taa zimeshuka na kuwapa Wakenya tumaini jipya la maisha baada ya tathmini ya karibuni kabisa ya Mamlaka ya Nishati na Petroli (EPRA).

Bei za mafuta ya Petroli na Diseli zimeshuka kwa shilingi 5 kuanzia kesho Ijumaa usiku wa manane huku bei ya mafuta ya taa ikushuka kwa shilingi 7.28.

Punguo hilo la bei za mafuta ni moja wapo ya suala kubwa la kuratilisha bei za mafuta nchini Kenya.

Kufuatia punguo hilo la bei za mafuta, lita moja ya Petroli itauzwa shilingi 129.72 jijini Nairobi kutoka shilingi 134.72 kisha Diseli iuzwe shilingi 110.60.

Mafuta ya taa yatauzwa shilingi 103.54 kwa lita.

“Licha ya ongezeko la bei za mafuta, bei sahihi za mafuta kwenye vituo vya petrol zimepunzwa. Serikali itatumia vilivyo tozo za maendeleo ya Petroli kusaidia wateja kutokana na bei za juu,” EPRA imesema kwenye taarifa yake ya leo Alhamisi.

Serikali inatarajiwa kufidia wauza mafuta kwa makato kutoka kwa viwango vya wasambazaji na faida kwenye mzunguko mwingine wa tathmini ya bei za mafuta wa mwezi November 14, 2021 kutokana na fedha zinazopatikana kutoka kwa tozo za petrol.

Hazina ya taifa ilitumia shilingi bilioni 8.7 za Kenya kufidia wauza mafuta kati ya mwezi Aprili na Agosti mwaka huu wakati mkakati wa kuratilisha ulipoanza.

Mwandishi: Ancillar Masika Gari

Tarehe: 14.10.2021

Saa: 12 jioni

Mrejesho: Tutumie maoni yako

 

Leave a Comment