Cherono Kipkorir (9) akiwa na kombe la ushindi jumla baada ya kushinda kwenye mashindano ya NCBA Royal Nairobi Golf Club leg ya mwaka 2021. (Picha/Hisani)

Nairobi, Kenya

Klabu ya Gofu ya Ruiru ndiyo mwenyeji mpya wa makala ya 22 ya gofu yanayodhaminiwa na NCBA mwaka huu 2021, Jumamosi hii.

Jumla ya wachezaji  200 wa gofu wanatarajiwa kupambana kwenye mkumbo wa 72 kujitafutia tiketi kwenye nafasi tano zilizosalia kujazwa za fainali zitakazofanyika mwezi ujao katika klabu ya gofu ya Karen Country Club.

Droo ya Ruiru inafikisha jumla ya wachezaji 2,800 wa gofu walioshiriki mashindano hayo tangu uasisi wake chini ya ufanisi wa michuano hiyo katika msimu wake wa kwanza.

Jumla ya wachezaji 100 wa gofu wakiwemo washambuliaji watano hatari zaidi kutoka kwa kila pambano la 20 la watu wazima lililofayika wamefuzu kwa ajili ya fainali hizo.

Kati ya 100 hao, watatu watakuwa wachezaji chipukizi walioibuka washindi jumla katika vilabu vyao vya Karen, Limuru na Royal Golf.

Mashindano ya pili ya wachezaji chipukizi wa gofu yatafanyika katika klabu ya gofu ya Muthaiga kuanzia tarehe 9 hadi 10 mwezi Disemba mwaka huu 2021.

Akizungumza juu ya mashindano hayo, Mkurugenzi wa NCBA , John Gachora amesema:

“Tunafurahia kupeleka mashindano yetu ya gofu Ruiru kwa ajili ya sherehe yetu ya mwisho ya mwaka huu. Hili ni tukio muhimu na la kujivunia sana kwetu sote NCBA kuona mashindano hayo katika kilele chake. Tunashukuru kila mmoja aliyewezesha mashindano haya kufaulu na tunasubiri kwa hamu kuona changamoto inayotusubiri Jumamosi hii.”

Mwandishi: Samuel Kombe Karisa

Tarehe: 18.11.2021

Saa: 9 alasiri

Mrejesho: Tupe maoni yako

Leave a Comment