Maguire na Arnold kukosa ngarambe za kufuzu kombe la dunia

LONDON.

Nahodha wa Manchester United, Harry Maguire, na beki wa Liverpool, Trent Alexander-Arnold, hawtajumuishwa kwenye kikosi cha timu ya soka ya Uingereza kwa michuano ya kufuzu kombe la dunia mwakani.

Wawili hao wana majeraha yaliyowakosesha ngarambe za Klbau bingwa barani Ulaya dhidi ya Villareal na FC Porto mtawalia katikati mwa juma hili.

Kwa mujibu wa meneja wa United Ole Gunnar Solskjaer, Maguire anatarajiwa kusalia mkekani kwa wiki kadhaa baada ya kuumia msuli wa mguu wikendi jana kwenye mechi dhidi ya Aston Villa.

Kwa upande wa, Alexander-Arnold anauguza jeraha la kinena na hajulikani atarejea lini ugani.

Kocha wa Uingereza Gareth Southgate anatarajiwa kutaja kikosi chake cha mpambano dhidi ya dhidi ya Andorra na Hungary leo Septemba 30, 2021.

Uingereza waliotinga fainali ya Euro 2020 na kuzidiwa ujanja na Italia, wameratibiwa kuvaana na Andorra ugenini Oktoba 9 kabla ya kuvaana na Hungary Oktoba 12 ugani Wembley.

Leave a Comment